Masharti ya Matumizi
Imesasishwa: Oktoba 2026
Kwa kutumia Singeli App unakubali masharti haya.
Akaunti
Unawajibika kwa usalama wa akaunti yako na kila kinachofanyika ndani yake.
Maudhui unayopakia
- Unapakia tu kazi unazozimiliki au una ruhusa ya kuzisambaza.
- Hairuhusiwi maudhui ya chuki, matusi makali, ulaghai au yanayovunja sheria.
- Unaendelea kumiliki kazi zako; unatupa ruhusa ya kuzionyesha na kuzicheza kwenye app.
Malipo
Baadhi ya huduma (kupakia nyimbo, video, EP, beats na matangazo) zinalipiwa kwa simu. Malipo yaliyokamilika hayarudishwi isipokuwa kama huduma haikutolewa.
Beats, kolabo na studio
Mikataba kati ya wasanii, ma-producer na studio ni kati yao wenyewe. Singeli App si mhusika wa makubaliano hayo.
Kusitisha
Tunaweza kuondoa maudhui au kusimamisha akaunti inayovunja masharti haya.
Wasiliana nasi
admin@singeliapp.com